Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCEF yatoa msaada kwa zaidi ya familia 5000 kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati

UNCEF yatoa msaada kwa zaidi ya familia 5000 kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linatoa misaada ya dharura kwa zaidi ya watu 5,500 ambao wamelazimika kuhama makwao kwenye maaeno yaliyo kaskazini mwa Jamahuri ya Afrika ya Kati.

Asilimia kubwa ya wale waliohama makwao ni  wanawake na watoto ambao sasa wanaishi katika mazingira mabaya wakiwa hawana maji wala makao. Karibu watu 400,000 wanaripotiwa kuhama makwao kaskazini magharibi mwa nchi. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARXIE MERCADO)

“Timu ya UNICEF inatoa msaada wa dharura kwa takribani familia 5500 zilizoathirika machafuko ya karibuni Kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wengi wa wakimbizi hao wa ndani ni wanawake na watoto ambao sasa wanaishi katika hali mbaya bila maji safi, wala malazi. Tathimini ya Umoja wa mataifa inaonyesha kwamba sasa kuna karibu watu 400,000 ambao wametawanywa na machafuko wakiwemi 170,000 ambao wametawanywa na mapigano ya karibuni Kaskazini Magharibi katika wiki za karibuni. Wengi wa watu hawa wamejificha vichakani kwa hofu. Na zaidi ya watu 60,000 wamekimbilia nchi jirani.”