Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugaidi usipodhibitiwa utaathiri ajenda ya maendeleo: Botswana

Ugaidi usipodhibitiwa utaathiri ajenda ya maendeleo: Botswana

Hatimaye mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefikia ukingoni hii leo kwa watoa hotuba kuzungumzia amani, ulinzi, usalama, mazingira na maendeleo duniani. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Siku ya mwisho ya mjadala mkuu, wajumbe walipokea ripoti kutoka kwa wawakilishi wa nchi na maeneo kama vileMaldives,Botswanana Holy See. Mathalani Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana Phandu Skelemani alitaja mafanikio ya utekekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia katika kutoa elimu ya msingi kwa wote na kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda mtoto. Akasema bado lengo namba saba ni changamoto kwani mabadiliko ya tabianchi yanaathirisanamazingira yaBotswana. Katika amani na usalama duniani akagusia ugaidi hukoKenya, Pakistani, mashambulizi Darfur na huko Nigeria na akaonya.

(Sauti ya Skelemani)

 “Vitendo hivi vya kigaidi ni tishio kwa amani na usalama duniani, na pia vinakwamisha jitihada za kimataifa za kujenga dunia yenye amani na ustawi. Hakuna shaka kuwa iwapo ugaidi wa kimataifa hautadhibitiwa, utaweza kudidimiza ajenda ya maendeleo ya dunia.”

 Visiwa vyaMaldivesviliwakilishwa na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Mariyam Shakeela yeye akasema mabadiliko ya tabianchi yanatishia mustakhbali wa taifahiloambalo asilimia 80 ya eneo lote liko mita moja na nusu juu ya usawa wa bahari na hivyo kutishia baiyonuwai muhimu inayotegemewa kwa uchumi na maendeleo ya nchi.

 (Sauti ya Dkt. Mariyam)

 “Maisha yetu yote ya kila siku, utamaduni, uchumi kwa kiasi kikubwa yanategemea biyonuwai ya bahari na ya pwani.  Kupotea kwa baiyonuwai hii kwa vyovyote vile kutasababisha madhara makubwa kwa Maldives”