Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eritrea yataka mfumo wa Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho

Eritrea yataka mfumo wa Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho

Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, Osman Mohamed Saleh ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa baraza hilo limepuuza maombi ya haki kwa nchi yake, tangu ilipoanza kufanya maombi hayo yapata miongo kadhaa ilopita.

Waziri huyo ambaye ameanza hotuba yake kwa risala za rambirambi kwa serikali na watu waKenyakufuatia shambulizi la jengo la Westgate mjiniNairobi, amesema, licha ya kupuuzwa huko,Eritrea inaamini kuwa kuendeleza haki za watu na matakwayao, pamoja na heshima miongoni mwa jamii ya kimataifa kutasalia kuwa mashakani bila shirika la kimataifa ambalo linalinda umuhimu.

Kama viongozi wengine wa Afrika, waziri huyo waEritreaametoa wito mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho.

 “Tunachotaka, kama wengine, kimekuwa na kitasalia kuwa, kuendeleza juhudi za kufanyia marekebisho Umoja wa Mataifa. Kama ilivyo, hali ya taifa letu inaashiria tu hali ilivyo katika Umoja wa Mataifa kwa ujumla, ambayo imekumbwa na udhaifu wa mara kwa mara na wingi wa dosari.”

Waziri Saleh amesema katika karne ya 21, Umoja wa Mataifa unatakiwa kurekebishwa ili uwe na nguvu zinazotokana na uanachama wa wake wa ulimwengu mzima, na wala siyo tu nchi moja au nchi chache kufanya maamuzi makubwa.