Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazitaka mamlaka za Iraq kurejesha utulivu mjini Erbil

UM wazitaka mamlaka za Iraq kurejesha utulivu mjini Erbil

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Iraq, Nickolay Mladenov, ameelezea kushtushwa na msururu wa milipuko ya mabomu ambayo yameulenga mji wa Erbil mnamo siku ya Jumapili na kusababisha vifo pamoja na kuwajeruhi watu kadhaa.

Bwana Mladenov amesema kwa miaka mingi, mji wa Erbil umefurahia amani na usalama.

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu ametoa wito kwa mamlaka za kikanda na kitaifa kushirikiana ili kuhakikisha kuwa hali inabakia kuwa tulivu, na wote walohusika katika kutekeleza mashambulizi hayo wanawajibishwa kisheria