Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya uchunguzi wa silaha za kemikali yaondoka Syria

Timu ya uchunguzi wa silaha za kemikali yaondoka Syria

Timu ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria ikiongozwa na Prof. Ǻke Sellström, imeondoka nchini Syria baada ya siku sita za kufanya uchunguzi nchini humo.

Timu hiyo sasa imekwenda kwenye hatua ya kuikamilisha ripoti yake, ambayo inatarajiwa kuwa tayari mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Wakati huo huo, Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amezungumza leo kwa njia ya video na kamati kuu ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, mjini Geneva, na kutaka yazingatiwe mahitaji ya zaidi ya wakimbizi wa Syria milioni 2.1 ambao ama wameandikishwa au wanasubiri kuandikishwa katika nchi tano jirani.

Amesema kuwa athari za tatizo la wakimbiz kwa nchi jirani zimekuwa kubwa, huku huduma za umma zikipata shinikizo kubwa.