Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Christina Aguilera, Yum kwenye kampeni ya kukabiliana na njaa

Christina Aguilera, Yum kwenye kampeni ya kukabiliana na njaa

Mshirika wa muda mrefu wa shirika la chakula duniani WFP, Yum Brands amezindua wiki hii kampeni ya kukabiliana na tatizo la njaa.

Kama sehemu ya kutia msukumo kwenye kampeni hiyo yenye shabaha ya kukusanya fedha kwa ajili ya WFP ili kuratibu miradi yake, Yum ameshirikiana na mwimbaji mashuhuri duniani Christina Aguilera.

Hatua hiyo inakuja katika wakati ambapo mwimbaji huyo akiwa na ziara nchini Rwanda ambako alitoa msaada wa chakula kwa makundi ya watoto.

Akizungumzia shabaha yake,Yum alisema kuwa anakusudia kuwashawishi watu wengi zaidi kuchangia fedha kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wanaotabika na njaa.