Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zisizozungukwa na bahari zajadili mustakhbali wao

Nchi zisizozungukwa na bahari zajadili mustakhbali wao

Mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu mustakabali wa nchi zinazoendelea ambazo hazijazungukwa na bahari umeanza mjini New York ambapo wawakilishi wanaangazia uhusiano kati ya nchi zao na zile zenye bahari na jinsi ya kutumia bahari hizo kwa usafirishaji wa watu na bidhaa.

Katika mahojiano na idhaa hii Mwakilishi wa kudumu wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Tekela Alemu ambaye anaiwakilisha nchi yake kwenye kikao hicho amezungumzia matarajaio ya nchi yake.