UNHCR yazidiwa uwezo katika kusaidia wakimbizi

30 Septemba 2013

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema mwaka huu wa 2013 umeshuhudia idadi kubwa zaidi ya watu wakikimbia makwao kwa sababu mbali mbali kuliko kipindi chochote kile ndani ya karibu miongo miwili, na hivyo kufanya shirika hilo lishindwe kutoa usaidizi unaotakiwa. Ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

UNHCR inasema kuwa katika kipindi cha mwaka huu pekee, zaidi ya raia milioni 1.5 wa Syria wamekimbilia nchi za nje, huku wengine maelfu kwa maelfu wakiwa wamekwamba majumbani mwao katika nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, Sudan, Mali na Somalia.

Akizungumza mjini Geneva, kamishna na UNHCR Antonio Guterres  amesema kuwa ustawi wa wakimbizi hao ni mbaya kutokana na kukosa huduma za usamaria mwema.

Bwana Guterres ameeleza kuwa tatizo la wakimbizi wa Syria linaweza kuzusha janga kubwa la kieneeo na hivyo ametoa wito kwa pande zinazopigana kusaka ufumbuzi wa mazungumzo ya kisiasa.

 (SAUTI YA GUTERRES) TAFSIRI PIA

“Mzozo huu unapaswa kukoma.Kama raia wa dunia, nimekerwa na kuchoshwa kuona wito wa kutaka kupatikana kwa suluhu ya kisiasa, wito huu unaangukia masikioni mwa viziwi na pande zote zimeshindwa kukaa meza moja kumaliza mzozo unaogharimu maisha ya waSyria wengi ambao pia unanyemelea katika mataifa ya jirani.

Kwa upande mwingine Bwana Guterres amezipongeza nchi zinazoendelea kutoa hifadhi wa wakimbizi hao wa Syria na akataika jumuiya ya kimataifa kuwa sehemu ya usaidizi wa wakimbizi hao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter