WHO, FAO na OIE waungana kutokomeza kichaa cha mbwa:

WHO, FAO na OIE waungana kutokomeza kichaa cha mbwa:

Shirika la afya duniani WHO, shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la afya kwa ajili ya afya ya mifugo OIE wameungana kwa nia ya kutokomeza kabisa kichaa cha mbwa kwa binadamu na kudhibiti ugonjwa huo kwa mifugo. Watu zaidi ya 60, 000 hufa kila mwaka kutokana na kichaa cha mbwa.

Tarehe 28 septemba kila mwaka ni siku ya kichaa cha mbwa. Kwa mujibu wa mashirika hayo matatu ni fursa kwa kila mmoja kujifunza zaidi kuhusu kichaa cha mbwa na kuimarisha juhudi za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo. Ingawa kichaa cha mbwa kinaweza kuzuilika lakini kinauwa maelfu ya watu kila mwaka. na watu wanne kati ya 10 wanaokufa na kichaa cha mbwa ni watoto.

Hii ni mara ya kwanza mashirika haya matatu ya WHO, FAO na OIE yametoa taarifa ya pamoja yakiahidi kutokomeza kabisa ugonjwa huo kwa binadamu na kuudhiti miongoni mwa wanyama.