Skip to main content

Ban akutana na kuzungumza na rais wa Mali

Ban akutana na kuzungumza na rais wa Mali

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameendelea kukutana na wakuu mbalimbali wa nchi na kufanya nao mazungumzo ambapo leo amekutana na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita.

 Katika mazungumzoyao Katibu Mkuu ameelezea masikitiko yake kufuatia shambulio katika eneo liitwalo Timbuktu lililosababisha vifo na majeruhi  kadhaa. Amesema tukiohilolinaonyesha dhahiri umuhimu wa kuimarisha usalama Kaskazini mwa nchi.

 Bwana Ban amesema suluhisho la kudumu ni kuunda upya sekta ya usalama, kuimarisha utawala na kuanzisha mamalaka ya kiserikali Kaskazini .

 Katibu Mkuu Ban amesisitiza utayari wa UM kupitia ujumbe wake wa kuimarisha amani nchiniMali, MINUSMA ili kuwasaidia serikalia ya Mali na watu wanaokutana na changamoto hizi

 Kadhalika ameelezea msaada wa UM kwa ajili ya amani jumuishi na uratibu wa uchaguzi wa kisheria. Bwana Ban pia amesisitiza umuhimu wa jumuiya ya kimataifa kuwa na mewlekeo mmoja kwa ajili ya ukanda wa Sahel.