Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limeweka historia: Ban awaeleza waandishi wa habari

Baraza la Usalama limeweka historia: Ban awaeleza waandishi wa habari

Ni siku ya kihistoria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliwaeleza waandishi wa habari punde baada ya baraza la usalama kupitisha azimio kuhusu uteketezaji wa silaha za kemikali zaSyria. Hata hivyo amesema kuteketeza silaha za kemikali kwenye nchi iliyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kazi kubwa lakini wanashirikiana na OPCW kuandaa mfumo wa kufanya hivyo haraka na kwa usalama na kwamba hilo litajidhihirisha kwenye mapendekezo yake kwa Baraza la Usalama siku za usoni. Bwana Ban amesema msingi wa amani kwaSyriasasa umeanza kujengeka kutokana na uamuzi huo wa Baraza la usalama wa kuridhia makubaliano yaGenevana kwamba amewaeleza wajumbe kuwa matarajio ya mkutano wa pili waGenevakuhusuSyriani katikati ya mwezi Novemba. Alipoulizwa anaweza kukutanisha Rais Bashar Al Assad na wapinzani ili kuanzisha mchakato wa  kipindi cha mpito Bwana Ban amesema upande wa upinzani unapaswa kuwa na ujumbe mmoja ukiwakilisha sauti za wasyria walio ndani na nje ya nchi yao na kwamba makubaliano ya mwaka jana ya Geneva yameweka dhahiri mchakato huo.