Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Baraza Kuu la UM ukishika kasi, Viongozi wa Afrika watathimini malengo ya milenia

Mkutano wa Baraza Kuu la UM ukishika kasi, Viongozi wa Afrika watathimini malengo ya milenia

Tarehe 24 mwezi huu wa Septemba mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulianza rasmi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Wakuu wa nchi, marais na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa umoja huo wanashiriki katika mjadala huo utakaomalizika tarehe Pili mwezi ujao. Je Afrika Mashariki ilikuja na ajenda gani? Viongozi walisema nini? Basi ungana na Joseph Msami katika makala hii.