Suala la tindikali laibuka kwenye mazungumzo kati ya Ban na Rais Kikwete

27 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambapo ametoa shukrani kwa mchango wa nchi hiyo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO na kule Darfur, UNAMID. Katikahilo, viongozi hao wawili wameelezea masikitikoyaokufuatia vifo vya walinda amani waTanzaniana wamejadili uwezo wa kikosi cha kujibu mashambulizi huko DRC. Halikadhalika wamebadilishana mawazo kuhusu uhusiano kati yaTanzaniana nchi jirani pamoja na ushiriki waTanzaniakwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mwakani. Bwana Ban pia amegusia suala la mashambulizi ya tindikali hukoZanzibarpamoja na hali ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchiniTanzania.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter