Ban asikitishwa na ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi

27 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amekaribisha ripoti ya tathmini ya tano ya jopo la kiserikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCC na kusikitishwa na matokeo yake.

Ripoti hiyo inaweka dhahiri kuwa madhara anayosababisha mwanadamu kwenye mfumo wa tabianchi ni bayana katika maeneo mengi ya dunia, na inawezekana kuwa madhara hayo alosababisha mwanadamu yamekuwa ndiyo makubwa zaidi kwa ongezeko la joto duniani tangu kati mwa karne ya 20.

Bwana Ban amesema kupunguza mabadiliko ya tabianchi kutahitaji kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi chafuzi za greenhouse na kwa njia endelevu. Katibu Mkuu ametoa wito kwa nchi zote kufanya kila juhudi inayohitajika ili kufikia mkataba wa kimataifa wa sheria kuhusu hali ya anga ifikapo mwaka 2015, na kuchukuwa hatua haraka kupunguza athari zake.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter