Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa:Figures

27 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christiana Figures na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wamesema matokeo ya utafiti wa karibuni wa ripoti ya IPCC kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni wito wa wazi kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha juhudi za kupamana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuondoa binadamu katika eneo la hatari.

Leo Ijumaa jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa linalojadili mabadiliko ya hali ya hewa IPCC limetoa awamu ya kwanza ya tathimini ya ripoti yake ya tano kuhusu sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti inaonyesha kwamba kuna mchango mkubwa wa binadamu katika mabadiliko ya hali ya hewa kuliko wakati mwingine wowote. Akizungumzia hilo kwenye baraza kuu mjini New York Bi Figures amesema

sote tunafahamu juhudi za kuzuia ongezeko la joto duniani hazitoshi kwa kiwango kinachohitajika hkuondoa maisha ya binadamu hatarini, serikali lazima zichukue hatua na kuandaa agenda 2015 ambayo itasaidia kuchapuza hatua za kimataifa

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter