Angola yamulika amani DRC, yataka marekebisho ya muundo wa Baraza la Usalama

27 Septemba 2013

Suala la amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni miongoni mwa mambo yaliyokuwemo kwenye hotuba ya Makamu wa Rais wa Angola Manuel Domingos Vicente aliyotoa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos. Bwana Vicente amesema hali eneo hilo linatishia usalama siyo tu wakazi wa eneo hilo bali pia ukanda mzima. Amesema ni lazima kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya ulinzi, amani na usalama kwa DRC yaliyotiwa saini huko Addis Ababa mwezi Februari mwaka huu ambayo amesema ndio mfumo sahihi wa kupatia amani ya kudumu eneo hilo.

(Sauti ya Vicente)

Angola nayo ikapaza sauti kuhusu muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikisema…..

(Sauti ya Vicente)

Mizozo ya Syria na Misri pia aliizungumzia na kusema kutaka jumuiya ya kimataifa chini ya uongozi wa Umoja wa Kimataifa kupatia suluhu la kudumu mizozo hiyo inayozidi kuathiri raia wasio na hatia.