Migogoro nchini Mali inatokana na hali ngumu ya maisha:Rais Keita

27 Septemba 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo katika siku ya nne hii leo viongozi wameendelea kuhutubia wakijikita katika masuala ya ulinzi, amani usalama na maendeleo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Akitoa hotuba yake wakati wa mjadala mkuu wa Baraza Kuu, Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubakar Keita amewasilisha shukrani za watu wa nchi yaMalikwa jamii ya kimataifa katika kusaidia kuerejesha amani na usalama nchini humo.

Kwenye hotuba hiyo ilojaa shukran kem kem, Bwana Keita ameshukuru kwa ujumla kazi ya Umoja wa Mataifa, likiwemo Barza la Usalama katika kupitisha maazimio muhimu ambayo yamesaidia kukabiliana na makundi ya wanamgambo wa Jihad, na kulishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa mchango wake, na kutaja nchi mbalimbali za Afrika kwa kuchangia kurejesha utulivu nchini Mali.

 Akiongea kuhusu hali kwa ujumla nchiniMali, Bwana Keita amesema migogoro nchini humo imetiokana na hali ngumu za maisha.