Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuanza utekelezaji wa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia ni muhimu:Ban

Kuanza utekelezaji wa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia ni muhimu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema hatua zimepigwa tangu mkutano wa mwaka 2011 wa kuhusu kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia. Amesema nchi tano mpya zimejiunga katika mkataba huo ili kufanikisha nia ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia.

Amezipongeza nchi hizo ambazo ni Brunei, Chad, Guatemala, Guinea-Bissau, Indonesia na Iraq kwa kuchukua hatua jiyo muhimu. Sasa mkataba huo wa kupinga majaribio ya nyuklia una nchi 160 zilizouridhia.

Ban amesema katika mkutano wa ngazi ya juu kando ya majadala wa baraza kuu kuhusu upokonyaji wa silaha wametoa wito wa kutaka mkataba huo kuanza kufanya kazi mara moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Marufuku ya majaribio ya nyuklia ni hatua muhimu katika kuelekea kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia. Na ni njia pekee inayokidhi matumaini ya watu walioathirika saana na uzalishaji , majaribio na matumizi ya silaha hizi”

Ban amewatolea wito wajumbe wote wa jumuiya ya kimataifa kumaliza mkwamo katika mchakato wa upokonyaji silaha, na kuwataka kuhakikisha mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia unaanza kufanya kazi na kuchukua hatua zaidi ya kuwa na dunia bila silaha za nyuklia.