Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na kifo cha mlinda amani wa Tanzania DRC:

Ban asikitishwa na kifo cha mlinda amani wa Tanzania DRC:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amestushwa na kifo cha mlinda amani wa Kitanzania ambaye alijeruhiwa kwenye mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwisho wa mwezi Agost.

Mlinda amani huyo alijeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia eneo la Umoja wa Mataifa karibu na milima ya Kibati Kaskazini mwa Goma. Mlinda amani huyo ni Mtanzania wa pili kufariki dunia kutokana na shambulio hilo.

Katibu Mkuu amelaani vikali kuwauwa na kuwajeruhi walinda amani wa MONUSCO na ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kwa serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania.

Umoja wa mataifa unaendelea kuchukua hatua zote muhimu kuzingatia azimio la baraza la usalama namba 2098 la mwaka 2013 la kuwalinda raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.