Wachunguzi wa UM wa silaha za kemikali Syria wanafanyia kazi ripoti ya mwisho.

27 Septemba 2013

Tume ya Umoja wa mataifa inayochunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria Ijumaa imeendelea kuifanyia kazi ripoti ya mwisho ambayo inatarajia itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Oktoba. Flora Nducha na ripoti kamili

 (RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Ripoti hiyo inatokana na madai mbalimbali yaliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na saba kati ya madai hayo ymebainika kuhakikisha uchunguzi huo kwa mujibu wa mfumo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchunguzi wa madai ya matumizi ya silaha za kemikali na baiolojia.

Madai ya matumizi ya silaha hizo yanatokana na matukio saba ya mwaka huu yaliyoripotiwa.

Tume ya uchunguzi ambayo ilirejeaS yria kwa kazi ya pili Septemba 25 inatarajia kukamilisha shughuli zake nchini humo Jumatatu Septemba 30. Tume hiyo inayoongozwana DrSellstrom inajumuisha wataalamu kutoka shirika la kupinga matumizi ya silaha za kemikali OPCW na Umoja wa Mataifa.