Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kuzungumza na waziri mkuu wa Ethiopia

Ban akutana na kuzungumza na waziri mkuu wa Ethiopia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU.

Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru kiongozi huyo wa Ehtiopia kwa namna nchi yake ilivyowezesha upatanishi huko Jubaland Somalia.

Viongozi hao walijadili hatua za kuimarisha amani nchini Somalia pamoja na kubadilishana mawazo juu ya ukwepaji wa sheria na haki za kimataifa