Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu Sierra Leone kwa kifungo cha Taylor

Ban akaribisha uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu Sierra Leone kwa kifungo cha Taylor

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kwa ajili ya Sierra Leone, wa kutupilia mbali ombi la rufaa la rais wa zamani wa nchi hiyo, Charles taylor, la kutaka kifungo chake cha miaka 50 ipinduliwe.

Kwa kauli moja, mahakama hiyo maalum ya rufaa iliamua kushikilia makosa yote kumi na moja ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu dhidi ya Charles Taylor, na kuidhinisha kifungo cha miaka 50 alichohukumiwa na mahakama ya chini mnamo Aprili 26 2012.

Akipongeza uamuzi huo, Bwana ban amesema hii ni siku kubwa katika historia kwa watu wa Sierra Leone na ukanda mzima, na kuongeza kuwa uamuzi huo ni hatua kubwa katika mfumo wa kisheria wa kimataifa, kwani unathibitisha kifungo cha kiongozi wa taifa wa zamani kwa makosa ya kusaidia na kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Amewapa hongera wote katika mahakama hiyo kuhusu Sierra Leone kwa ufanisi huu muhimu, na kuwashukuru kwa kujitoa kuhakikisha uwajibikaji kwa ajili ya uhalifu mbaya zaidi ulotekelezwa wakati wa mgogoro nchini Sierra Leonne.