Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na vifo vya tetemeko la ardhi Pakistan:

Ban asikitishwa na vifo vya tetemeko la ardhi Pakistan:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesem amesikitishwa na maisha ya watu yaliyopotea nchini Pakistan kutokana na tetemeko la ardhi. Tetemeko la ukuwa wa vipimo vya rishta 7.8 lililikumba eneo la Balochistan tarehe 24 Septemba na kusababisha uharibifu mkubwa , huku likibomoa maelfu ya nyumba na kupoteza maisha ya watu.

Ban ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Pakistan hususani kwa familia za waliouawa kwenye tetemeko hilo na kuathirika pia. Ban amesema Umoja wa mataifa uko tayari kutoa msaada wowote katika juhudi za kuwasaidia walioathirika kwa misaada ya kibinadamu kutokana janga hilo. Pia ameongeza kuwa Umoja wa mataifa uko tayari kukusanya msaada wa kimataifa kama utahitajika.

.