Viongozi wa Afrika wazungumzia ukuaji wa uchumi katika bara lao:

26 Septemba 2013

Wakilaani vita vinavyoendelea Syria na kwingineko viongozi wa dunia ambao wamewasilisha ripoti zao wameelezea na kupongeza ushirikiano baina ya amani na maendeleo katika mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambao leo umeingia siku ya tatu.

Rais Joseph Kabila Kabange wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema usalama unasalia kuwa kitovu muhimu cha maendeleo na bila amani itakuwa ndoto kupata maendeleo hayo. Kwa upande mwingine amani barani Afrika inahitaji mipango ya maendeleo ambayo itatoa suluhu ya hali ya sintofahamu kwa watu masikini na kwa hali ya uchumi wa kimataifa amesema Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso akisisitiza kwamba nchi yake ambayo haina bahari ina mpango wa kukuza uchumi na kuhakikisha maisha bora kwa watu wake.Wengi wa viongozi takriban 30 ambao tayari wamezungumza wametanabaisha kuhusu ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Rais Macky Sall wa Senegal amesema kushuka kwa msaada maalumu wa maendeleo ODA hakukidhi mahitaji ya nchi za Afrika na mchakato wa hatua zinazowafanya kutafuta njia mbadala za vyanzo vya kifedha na miradi ya maendeleo. Amesema bara la Afrika sio tena anfa za machafuko na mahitaji ya dharira ya kibinadamu , lakini ni eneo linalochipukia na kuwa na fursa na uwekezaji.

Kwa Ivory Coasyt Rais Alassane Ouattara amesema kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia imekuwa kikwazo lakini anashukuru mchipuko wa uchumi nchini mwake ambao unalisongesha mbele taifa hilo na kuanza kupiga hatua. Amesema serikali imepitisha mipango ya kitaifa ya ujenzi kwa mwaka 2012 hadi 2015, kwa lengo la kuunda nafasi 200,000 za ajira kila mwaka hii ni idadi kubwa ukilinganisha na ukubwa wa eneo la nchi hiyo.

.