Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Pohamba asifu kazi ya kikosi cha UM cha kulinda amani DRC

Rais Pohamba asifu kazi ya kikosi cha UM cha kulinda amani DRC

Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo umeingia siku ya tatu kwa hotuba za viongozi mbali mbali wakigusia masuala ya amani, maendeleo na haki za binadamu wakiangazia ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015. Assumpta Massoi amefuatilia na hii ni taarifa yake.

(Taarifa ya Assumpta)

Kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kuhutubia hii leo alikuwa Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba ambaye alisema nchi yake inafuatilia na kushiriki kwa makini kwenye jitihada za kuleta amani duniani. Amegusia Madagascar na maandalizi yake ya uchaguzi akitaka usaidizi wa hali na mali ili uchaguzi uweze kufanyika na wananchi waweze kutekeleza haki hao ya kidemokrasia. Akagusia pia Somalia akisema jitihada za amani ziendelee kuungwa mkono na kwa Zimbabwe akataka vikwazo vyote dhidi ya nchi hiyo viondolewe bila masharti yoyote. Kuhusu Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC amepongeza kazi inayofanwa na Umoja wa Mataifa kuleta amani hususan kupelekwa kwa kikosi cha kujibu mashambulizi kutoka kwa waasi.

(Sauti ya Rais Pohamba)