Baraza Kuu laangazia utokomezaji wa silaha za nyuklia, Iran yazungumza

26 Septemba 2013

Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu suala la kutokomeza silaha za nyuklia na kupunguza silaha kwa ujumla. Joshua Mmali amekuwa akiufuatilia mkutano huo.

TAARIFA YA JOSHUA

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, John William Ashe, ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, kuwekeza sehemu ya rasilmali ambazo zinapatikana kutokana na utekelezaji wa mikataba ya kuondoa na kupunguza silaha katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Bwana Ashe amesema hayo wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu, ambao umeangazia suala la utokomezaji wa silaha za nyuklia. Rais huyo wa Baraza Kuu amesema dunia inayomiliki silaha za uangamizaji si salama, na wala haiwezi kusaidia upatikanaji wa amani na usalama kwa wote.

Tunapoweka muda, rasilmali na juhudi zetu katika kudumisha na kuendeleza silaha kali, tunahamisha rasilmali kutoka kwa elimu, huduma za afya, kupunguza umaskini, na kwa ujumla, lengo la kuendelea kufikia maendeleo endelevu. Je, si ni kinaya cha kuhuzunisha ya kwamba, tunapowekeza rasilmali zetu katika kuboresha maisha ya watu kote duniani, tunazingatia zaidi na kuwekeza katika vyombo vya kuwaangamiza?

Taifa la Iran limekuwa likikabiliwa na tuhuma kwamba linaendeleza mpango wa silaha za nyuklia. Akiongea kwenye mkutano wa leo, Rais mpya wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa dunia yenye amani na usalama ni kitu ambacho kinafaa kuaziziwa na kila mtu.

.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter