Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nchi 100 zaahidi kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kingono na ubakaji vitani:

Zaidi ya nchi 100 zaahidi kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kingono na ubakaji vitani:

Azimio lililozinduliwa kando ya mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York lina miakakati ya ya vitendo na kisiasa ya kutokomeza matumizi ya ubakaji na ukatili wa kimapenzi kama silaha ya vita.

Nchi 113 zimeidhinisha azimio la kihistoria la kubeba jukumu la kumaliza ukatili wa kimapenzi katika migogoro. Nchi nyingine zinaendelea kuwa na fursa ya kuidhinisha azimio hilo hadi tarehe 4 Oktoba. Zainab Bangura ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye vita

(SAYTI YA ZAINAB BANGURA)

Uwepo wenu hapa leo unatuma ujumbe kwa waathirika kote duniani, kwamba jumuiya ya kimataifa haitokaa kimya kuona miili yenu inatumika kama uwanja wa mapambano kwa faida za kisiasa na kijeshi.Siku ambazo ukatili wa ngono katika vita kuchukuliwa kama bahati mbaya ya matokeo ya vita zimekiwsha.Sasa kwa kuwa tumebadili mtazamo ni lazima pia tuzuie na kukomesha vitendo hivi.