Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea ukomo MDGS, elimu ya msingi yaboreshwa Tanzania

Kuelekea ukomo MDGS, elimu ya msingi yaboreshwa Tanzania

Wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukiendelea mjini New York huku mjadala mkuu ukiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia , Tanzania imepiga hatua katika lengo la pili la elimu kwa wote ambapo takwimu zinasema mwaka jana uwiano wa uandikishaji wa wavulana ulikuwa asilimia 14.4  huku wasichana ikiwa aslimia 97.3

Mkoani Ruvuma nchini humo pia mafanikio makubwa yanatajwa katika kiwango cha kuongeza idadi ya wanaojiandikisha shule ya msingikamamakala iliyoandaliwa na Enes Mwaisakila na Tamimu Adam kutoka radio washirika  Jogoo Fm ya Ruvuma nchini Tanzania inavyofafanua.