Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yatimiza lengo la kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano:Mwinyi

Tanzania yatimiza lengo la kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano:Mwinyi

Serikali ya Tanzania imesema inajivunia kutanabaisha kwamba lengo la nne la milenia ambalo ni kupunguza vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano limetimizwa tayari ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.

Akizungumza na Flora Nducha wa Radio ya Umoja wa Mataifa waziri wa afya wa nchi hiyo Dr Hussein Mwinyi amesema na kwa malengo mengine mawili ya afya yaliyosalia wamepiga hatua kubwa

(SAUTI YA DR HUSSEIN MWINYI)