Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya haki za binadamu nchini Sudan yasalia kuwa mbaya:UM

Hali ya haki za binadamu nchini Sudan yasalia kuwa mbaya:UM

Hali ya haki za binadamu nchini  Sudan  inasalia kuwa mbaya huku raia wakinyimwa fursa ya kufurahia haki zao zikiwemo za kisiasa kwa mujibu wa mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Mashood A. Baderin ambaye ni mtalaamu anayehusika na hali ya haki za binadamu nchini Sudan amesema kuwa kubana shughuli za mashirika ya umma, vyombo vya habari, kushika na kuzuilia na kubana haki za kidini nchini Sudan ni ukiukaji wa haki za binadamu. Amesema kuwa hali ya usalama kwenye maeneo yanayokumbwa na mizozo kwenye jimbo la Darfur na Kordofan Kusini pamoja na jimbo la Blue Nile ni mbaya na ukwepaji wa sheria ni tatizo la kila mara.

“Aprili mwaka 2013 serikali ilitangza kuwa wafungwa wote wa siasa wataachiliwa. Baahii ya wafungwa wa kisiasa waliachiliwa lakini haijabainika kuwa wafungwa wote wa kisiasa wameachiliwa. Mwezi mmoja baadaye mnamo Mei mwaka 2013 serikali ilitangaza kiviacha huru vyombo vya habari hata hivyo magazeti kadha yamebaki yamefungwa. Kwenye ripoti yangu naishauri serikali kutimiza ahadi yake ya kuwaachilia wafungwa wote wa kisiasa walio bado kizuizini  na kutangaza hili kwa umma. Nyingi ya changamoto zilizotajwa zinatokana na oparesheni za idara ya usalama wa taifa. Nimesisitiza kwenye ripoti yangu wajibu wa serikali na makundi ya waasi kulinda haki za binadamu wakati  wa mizozo. Nimesisitiza umihimu wa kumaliza mizozo Darfur, Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile kwa kuwa mizozo ndiyo chanzo cha ukiukaji wa haki za binadamu sehemu hizo za Sudan.”

Amesema kuwa karibu raia 300,000 wamekimbia makwako kati ya mwezi Januari  na Aprili mwaka huu kwenye eneo la Darfur.