Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNCTAD kushusu sheria za biasharakwa njia ya mtandao za ASEA yachapishwa

Ripoti ya UNCTAD kushusu sheria za biasharakwa njia ya mtandao za ASEA yachapishwa

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD imeelezea hatua kubwa zilizopigwa na nchi za eneo la Kusin mwa Asia ASEAN ambazo zimefanikisha mpango wa biashara kwa njia ya mtandao yaani e-commerce.

Ripoti hiyo yenye kichwa cha habari,mapitio ya sheria katika eneo la ASEAN imependekeza kuharakisha mchakato wa muungano wa kikanda ili kufanikisha mpanago wa ICT wa mwaka 2015 George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE)

Biashara kwa njia ya mtandao imetajwa kuwa ndiyo karata muhimu kwa nchi za eneo la Kusin mwaAsia kufanikisha agenda yake ya jumuiya ya ushirikiano ya kiuchumi.

Ripoti hiyo imesema kuwa, ni mihimu nchi wanachama zingazingatia kuimarisha soko la pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutapanua biashara na kuimarisha sekta za kiuchumi.

Nchi za eneo hilo zinatajwa kuwa ndizo za kwanza kuanzisha kile kinachoitwa ulingano wa msuala ya kisheria kwa ajili ya kufanikisha agenda ya biashara mtandao.Hata hivyo ripoti imezihimiza nchi hizo kuwa waangalifu wakati zinatekeleza mpango huo wa sheria ya pamoja.

 Hata hivyo kuna hali ya kutolingana kuhusiana na upitishwaji wa sheria hiyo ya pamoja. Nchi zaMalaysia,PhilippinesnaSingaporezimepitisha sheria inayozingatia hali ya faragha kuhusiana na mitandao lakini sheria hiyo imepitishwa kwa kiwango kichache katika nchi zaIndonesianaViet Nam.

Sheria hiyo pia bado inajadiliwa katika nchi za Brunei Darussalam na Thailand.