Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutawashinda magaidi wa Al shabaab: Rais Museveni

Tutawashinda magaidi wa Al shabaab: Rais Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema watu waliohusika katika shambulizi la Nairobi na kuwaua raia wasio na hatia watasakwa na kuwajibishwa. Rais Museveni amesema hayo katika mahojiano maalumu na Radio ya Umoja wa Mataifa.

Mnamo mwaka 2010, Uganda iliathirika kwa mauaji ya mashambulizi ya mabomu, ambayo yalipangwa na kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab, ambalo pia limedai kuhusika katika shambulizi la Kenya mwishoni mwa wiki ilopita ambapo hadi kufikia sasa, zaidi ya watu 60 wameripotiwa kufariki dunia katika shambulizi hilo la Jumamosi.

(SAUTI YA MUSEVENI)