Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM ataka kufanyika kwa mashauriano ya kisiasa nchini Cambodia

Mjumbe wa UM ataka kufanyika kwa mashauriano ya kisiasa nchini Cambodia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini Cambodia Surya Prasad Subedi amesema kuwa kuwa taifa hilobado lina changamoto nyingi katika kuimarisha na kulinda haki za binadamu. Mjumbe huyo amesema kuwa hata kama uchaguzi wa hivi majuzi ulikuwa wa amani  serikali ilishindwa kuchunguza madai ya udanganyifu wakati wa shughuli hiyo  hali amboyo imeacha picha mbaya. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Ripoti ya jason)

Akilihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjiniGeneva bwana Subedi ameelezea wasi wasi wake kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani wakilalamikia matokeo ya uchaguzi mkuu wa wa Julai 28. Ametaka kufanyika mashauriano kati ya serikali na upinzani kupata susluhu la mzozo wa kisiasa unashuhudiwa nchini humo na kuliweka taifahilo kwenye mkondo wa kuelekea kwenye demokrasia.

(Sauti ya Subedi)

“Ninajutia kusema kuwa inaoenekana kwamba bado haijaeleweka nchini Cambodiia kuwa sehemu ya demokrasia ni kwa watu wote kuelezea maoni yao na wajibu wa nchi wakati wa maandano ya amani ni kusikiliza bali si kuwazuia. Baada ya kusema hili ninaendelea kuamini kuwa viongozi wa Cambodia bado wanaweza , na  wakati kama huu  kufanya uchaguzi huu kuwa kiungo muhimu katika safari ya kuifanya Cambodia kuwa taifa lenye usawa na lililo huru. Ni matumaini yangu kuwa wakati wa shughuli hiyo , hali hiyo itasuluhishwa bila ya kuwepo majeraha au kupotea kwa maisha na kwamba matakwa ya watu yataangaziwa kwenye mpango mpya wa serikali na kuilekeza nchi kwenye njia bora ya kidemokrasi.”