Uongozi bora na fedha kusaidia kutimiza lengo la elimu kwa wote:

25 Septemba 2013

Wakati duniani kote kuna watoto milioni 57 ambao hahudhurii shule ,suala la uongozi bora na ufadhili wa fedha ni muhimu saana ili kuwapa watoto wengi zaidi fursa ya elimu bora . Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alizindua mradi maalumu wa kimataifa wa elimu mwaka 2012 ili moja kumuingiza shule kila mtoto, pili kuimarisha ubora wa kusoma na tatu kuendeleza uraia wa kimataifa.

Mradi huo wa elimu wa kimataifa Jumatano Septemba 25 unaadhimisha mwaka mmoja na kwenye baraza kuu kuna mjadala maalumu wa bviongozi wa dunia wa kuangalia jinsi gain ya kuhakikisha lengo la milenia la elimu linatimia, lakini pia nini kifanyike baada ya mwaka 2015 na kujumuisha masuala ya uongozi bora na fedha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter