Malengo ya milenia yameleta ahueni kwa watoto, lakini wengi bado wanakumbwa na mkwamo: Ban

25 Septemba 2013

Matukio mbali mbali maalum yamekuwa yakiendelea sambamba na mjadala wa mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa na miongoni mwa matukio hayo hii leo ni kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo wake mwakani.  Flora Nducha na taarifa kamili

 (RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Tukio hilo liliandaliwa na Baraza Kuu ambapo Karibu Mkuu Ban Ki-moon katika hotuba yake amegusia masuala kadhaa ikiwemo uamuzi wa kijasiri wa kuridhia malengo hayo mwanzoni mwa karne ya 21 lakini akasema bado maendeleo yanakumbana na ubaguzi kwa misingikamavile jinsia, nafasi ya kiuchumi na hata mtazamo wa kijamii na zaidi ya watu Bilioni Moja ni mafukara.

Amesema hilo halifai kwani kwa kufanya hivyo ufikiaji malengo hayo kwa baadhi ya nchi utakwama. Hata hivyo amesema kuna mafanikio....

 (Sauti ya ban-1)

"Safari tuliyoanza mwaka 2000 imeshihudia tukiweka msingi thabiti kwa maendeleo zaidi.  Watoto waliozaliwamwaka huo hivi sasa wanaingia umri wa barobaro, wengi wao wakiwa na elimu, afya wanayohitaji kuanza maisha bora. lakini bado wengi wao hawana fursa hiyo. sasa wanapokaribia utu uzima na kadri jitihada zetu za maendeleo zinapoimarika, hebu basi tutambue jukumu lililo mbele yetu."

Katika kuelekea ajenda ya maendeleo baada ya 2015, Bwana Ban akasisitiza....

 (Sauti ya Ban-2)

"Ni lazima iwe thabiti kwa matarajio lakini iwe inaweza kutekelezeka kirahisi, ikipatiwa usaidizi na ubia mpya wa maendeleo. Ni lazima ajenda hiyo iwe ya dunia nzima lakini iweze kushughulikia matatizo magumu kulingana na mazingira na uwezo husika wa nchi. Ni lazima iheshimu haki hususan kwa wanawake, vijana na makundi ya pembezoni."