Ban atiwa hofu na hali nchini Maldives:

24 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa hofu na uamuzi wa mahakama kuu nchini Maldives wa kutoa amri ya kuahirisha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Septemba 28.

Amekumbusha kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Septemba 7 imetambulika kimataifa na kwa waangalizi wa kitaifa kama ulikuwa wa mafanikio. Amerejea wito wake kwamba ni muhimu saana matakwa ya wananchi yakaheshimiwa katika kuamua mustakhbali wa taifa hilo.

Huu ni uchaguzi muhimu katika kuhakikishia mchakato wa kidemokrasia nchini Maldives

Ban amesema watu wa Maldives wameonyesha ustahimilivu wa hali ya juu na ni lazima wawe na fursa bila kuchelewa ya kutimiza haki yao ya kupiga kura. Amewataka watu wote wan chi hiyo kujizuia , kuzingatia katiba na kufanya kazi pamoja katika kuweka mazingira ya amani na kufanya duru ya pili ya uchaguzi inayostahili haraka iwezekanavyo

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter