Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za maendeleo zikiengua baadhi ya maeneo, hazitakuwa endelevu: Zuma

Harakati za maendeleo zikiengua baadhi ya maeneo, hazitakuwa endelevu: Zuma

Harakati mpya za maendeleo duniani zaonekana kutenga na kudidimiza zaidi maeneo maskini duniani, hiyo ni kauli ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Ametaja mashauriano ya biashara, udhibiti wa mazingira kwa ajili ya kuinua uchumi kuwa baadhi ya viashirio vya kupuuzwa kwa maendeleo endelevu kwa maslahi ya maeneo hayo ikiwemo bara la Afrika. Rais Zuma amesema bila mazingira sawia kwenye shughuli za maendeleo endelevu ikiwemo uchumi shirikishi na jumuishi usiokuwa na egemeo la upande wowote, ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 haitaweza kufikiwa.

(Sauti ya Zuma)

Kuhusu shambulio la kigaidi nchiniKenyaamesema serikali yake itaendelea kutoa usaidizi wa ulinzi wa amani na ule unaohitajika katika kuleta amani  hukoSomalia. Akaenda mbali zaidi akagusia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema kuwa si la kidemokrasia, halina uwakilishi wa kutosha likiengua nchi maskini ambazo idadiyaoni kubwa ndani ya Umoja huo.

 (Sauti ya Zuma)