Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto za walemavu zitatimia iwapo kutakuwepo na dunia jumuishi: Wanyoike- Kibunja

Ndoto za walemavu zitatimia iwapo kutakuwepo na dunia jumuishi: Wanyoike- Kibunja

Zaidi ya watu Bilioni Moja duniani wanaishi na ulemavu, na Umoja wa Mataifa unasema kuwa kila uchwao vita na mizozo vinaongeza hatari ya idadi ya walemavu kuongezeka.  Hivyo basi, bila jamii jumuishi, maendeleo endelevu yatakuwa ni ndoto na hata ndoto za walemavu kuweza kuwa na maisha bora yenye hadhi haitaweza kufikiwa.

Katika kuhakikisha jamii hiyo inajumuishwa kando mwa mjadala mkuu wa Baraza kuu mjini New York, kulifanyika mjadala wenye maudhui ya kuwa ulemavu si kushindwa kufanya jambo na miongoni mwa washiriki ni Henry Wanyoike, mwanariadha mashuhuri mwenye ulemavu wa macho kutoka Kenya, akiwa na msaidizi wake Joseph Kibunja. Assumpta Massoi alipata fursa ya kuzungumza nao na kwanza Wanyoike alielezea lengo la uwepo wao.