Meli yenye chakula cha msaada kwa Wasyria yawasili Beirut

24 Septemba 2013

Meli iliyosheheni ngano kutoka Marekani yenye uwezo wa kuwalisha watu milioni 3.5 nchini Syria kwa kipindi cha mwezi mmoja imewasili mjini Beirut nchini lebanon ikiwa ni sehemu ya oparesheni ya dharura ya shirika lampango wa chukula duniani WFP. Alice Kariuki na taarifa kamili:

(TAARIFA YA ALICE)Meli hiyo inayofahamika kama MV Mathawee Nareee ilianza safari yake kutoka Houston jimbo la Texas nchini Marekani na kuwasili mjini Beirut tarehe ishirini mwezi huu na tani 22,000 za ngano ambapo tani 7000 zilizushwa mjini Beirut kabla ya meli hiyo kuelekea nchini uturuki na ngano iliyosalia ambapo ngano hiyo itasawa na kufarishwa kwa njia ya bahari kwenda nchini Syria. WFP inagawa unga wa ngano kwa maduka yanayopika mikate sehemu za mijini kabla ya kugawa mikate kwa watu wanaoihitaji. Kwenye maeneo ya Aleppo na Idleb shirika la mwezi mwekundu nchini Syria linasambaza mikate iliyopikwa kutoka kwa unga wa Shirika la WFP kwa watu waliahama makwao . Kwenye sehemu za vijijini WFP inasambaza unga moja kwa moja kwa familia ambazo zinajipikia mikate zenyewe wakati kila famiia ikiwa inapewa kilo 25 za unga ikiwemo pia misaada ya mafuta ya kupikia, maharagwe na sukari.