Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imechukua hatua kujumuisha walemavu: Wanyoike

Kenya imechukua hatua kujumuisha walemavu: Wanyoike

Wakati mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo New York, Marekani ajenda muhimu ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, mwanariadha mashuhuri kutoka Kenya mwenye ulemavu wa macho Henry Wanyoike amesema hatua zimepigwa kusaidia kundi hilo lakini bado kuna changamoto. Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii kando mwa mijadala inayoendelea New York, Wanyoike ambaye pia ni balozi mwema wa kamati ya kimataifa ya michezo ya olimpiki kwa walemavu ametaja mafanikio hususan nchini mwake akigusia ujumuishi katika michezo.

(Sauti ya Wanyoike)

Wainyoke akaenda mbali zaidi na kutaja mchakato wa kisiasa na uwakilishi.

(Sauti ya Wanyoike)

Kuhusu kuwezesha walemavu kupata huduma mbali mbali amependekeza kuondolewa ushuru kwa vifaa kama vile vya kusomea au kusikiliza na hata vya kuwawezesha kutembea.