Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Côte d’Ivoire

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Côte d’Ivoire

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon leo amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara.

Viongozi hao wamejadili mafanikio yaliyofikiwa na Côte d’Ivoire tangu kuzuka kwa mgogoro kabla ya uchaguzi nchini humo na muundo wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa umoja huo nchini Côte d’Ivoire UNOCI pamoja na hali nchini Guinea Bissau.

Kadhalika Bwana Ban amepokea mtizamo wa serikali wa nchi hiyo kuhusu wapinzani na kutaka nchi iendeleze juhudi katika haki za binadamu ,uwajibikaji iiwamo ukatili wa kijinsia na kingono.

Amempongeza Rais Ouattara, kwa uongozi wake katik jumuiya ya uchumi magharibi mwa Afrika , ECOWAS, na mchango wa Côte d’Ivoire kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA.

Katibu Mkuu huyo wa UM pia amesema ameichagua nchi hiyo kuwa kiongozi katika utekelezaji wa UM katika juhudi za kusaidia wale wanaorejea makwao kujenga maisha yao katika mazingira salama na mahitaji ya laziam ya kijamii.