Viongozi wakutana kuhusu amani DRC na ukanda wa Maziwa Makuu

23 Septemba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Kuna uwezekano wa kupata amani, usalama na ushirikiano katika eneo la Maziwa Makuu, licha ya changamoto nyingi za kiusalama na kibinadamu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani, usalama na ushirikiano  kwa ajili ya eneo la Maziwa Makuu, ambao umefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Ban amewaomba viongozi wa kimataifa walohudhuria mkutano huo kuitikia wito wa kutimiza ndoto hiyo kwa kuridhia na kutekeleza mapendekezo ya kikanda ya kuwezesha amani, usalama na ushirikiano kwenye ukanda wa Maziwa Makuu.

"Nilipozuru ukanda huo mwezi Mei na rais wa Benki ya Dunia, Dokta Jim Yong Kim, tulitaka kuonyesha uungaji mkono wetu kwa makubaliano ya mependekezo hayo. Tulisisitiza kuwa amani na maendeleo vinapaswa kwenda sambamba. Watu walijitokeza mitaani kuelezea matumaini na hofu yao. Mwanamke mmoja alishika bango lenye maneno: “Amani, amani, amani tafadhali!” Maneno yake yanawakilisha wito wa mamilioni ya watu katika DRC na nje, ambao wanataka utulivu na maendeleo. Nawategemea nyote kutusaidia kuitikia wito wao huo wa dharura."

 Naye Katibu Mkuu wa Muungano wa nchi za Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma, amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kwa kuuandaa mkutano huo wa ngazi ya juu kama moja ya hatua za kutekeleza makubaliano yalosainiwa mjini Addis Ababa mnamo mwezi Februari mwaka huu 2013. Amewashukuru viongozi wa kimataifa walhudhuria mkutano huo wa ngazi ya juu.

"Uwepo wenu hapa ni ushahidi wa kujali kwenu kuhusu amani kwa watu wa DRC, hususan wanawake na watoto, ambao ndio wanateseka zaidi katika migogoro. Waheshimiwa, hakuna shaka kuwa changamoto zilizopo zinahitaji kuendelea kujitoa kwa nchi za ukanda huo kwa dhati na kwa uendelevu. Ni dhahiri kuwa amani pekee haitatotosha. Inapaswa kwenda sambamba na maendeleo katika DRC na katika ukanda mzima."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter