ILO yatoa takwimu kuhusiana na kupungua kwa ajira za watoto

23 Septemba 2013

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO, imesema kuwa kiwango cha ajira ya watoto duniani kimepungua kwa wastani wa theluthi moj hatua ambayo inaashiria mafanikio katika siku za usoni

Kiwango hicho ambacho ni cha mara ya kwanza tangu mwaka 2000 kimepungua kutoka watoto milioni 246 hadi kufikia milioni 168. Hata hivyo ripoti hiyo imeseama idadi hiyo bado ni ndogo ikilinganishwa na shabaha iliyopo ya kutokomeza kabisa ajira kwa watoto ifikapo mwaka 2016. George Njogopa na taarifa kamili

(Taarifa ya George Njogopa)

Ripoti hiyo ambayo imechapishwa katika wakati kukitarajiwa kufanyika kongamano la kimataifa kuhusiana na ajira kw awatoto  mwezi ujao huko Brasilia nchini Brazil, imebainisha mwelekeo wa kupungua kwa ajira hizo.

Imesema kuwa  kiwango hicho cha ajira kwa watoto kilianza kupungua katika kipindia cha kuanzia mwaka 2008 na 2012 ambako takwimu za ajira hizo zilishuka kuanzia milioni 215 hadi 168.

Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya watoto hao wametumbukizwa kwenye ajira hatarishi zinazokwaza ustawi wa afya zao.Inaelezwa kwamba kiasi cha watoto milioni 85 wangali wakitumikishwa kwenye ajira hatarishi, kiwango ambcho kimeshuka ikilinganishwa na kile kilichorekodiwa mwaka 2000 kulikokuwa na watoto milioni 171.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Ryder amesema mweleko wa kukabiliana na tatizo la ajira za watoto uko kwenye mkondo sahihi lakini kasi yake bado ni ndogo mno.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter