Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye shambulizi la kigaidi nchini Kenya

Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye shambulizi la kigaidi nchini Kenya

Takriban watu 62 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa baada ya watu waliojihami wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al shabaab kushambulia jumba moja lenye maduka mengi kwenye mji mkuu waKenyaNairobi. Zaidi ya watu 1000 waliokolewa kutoka kwenye jumba hilo la Westgate ambapo pia hadi sasa watu kadha wanakisiwa kushikiliwa na magaidi hao. Jason nyakundi na taarifa zaidi.

 (RIPOTI YA JASON)

Kulingana na Shirika la msalaba mwekundu nchiniKenyani kuwa hadi sasa watu 62 wamethibitishwa kuuwa wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa  huku watu 69 hawajulikani waliko kufuatia shambulizihilola kigaidi ambalo limelitikiza taifa laKenyana kuushangaza ulimwengu kwa ujumla. Hawa ni baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye jumbahiloambao walifanikiwa kukimbia na haya ni yale walioyashuhudia

 (SAUTI ZA WANANCHI)

Magaidi hao wanaokisiwwa kuwa wangambo la kundi la Al shabaaab kutokaSomaliawalilivamia jumba la Westgate mwendo wa saa tano asubuhi siku ya Jumamosi ambapo walianza kuwafyatulia watu  waliokuwa kwenye shughuli zao risai kiholela . Jumbahilo lina zaidi aya maduka 80 na hutembelwa sanana watu walio na uwezo wa kifedha. Masaa machache baadaye rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia alimpoteza mpwa wake wakati wa uvamizi huo alilihutubia taifa akililaani shambulizi hilo.

 (SAUTI YA KENYATTA)

Jumba hilo kwa sasa limezingirwa vikosi vya jeshi la Kenya wanaojaribu kuwaokoa watu ambao bado wanakisiwa kushikiliwa mateka na magaidi hao huku milio ya risasi ikisikika mara kwa mara kutoka kwa jumbahilona moshi mweusi nao mara nyingine ukionekana kutoka kwenye paa la jumbahilo.

Wakati hayo yakijiri mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imemruhusu makamu wa raias wa Kenya William Ruto ambaye amekuwa mjini Hague tangu juma lililopita akihudhuria kusikilizwa kwa kesi inayomkabili kuhusiana na uhalifu wa kivita kurudi nyumbani kwa kipindi ya juma moja baada ya yeye kutoa ombi la kutaka kurudi nyumbani kushughulikia hali iliyo sasa nchini Kenya baada ya kutokea kwa shambulizi la kigaidi.