ICC yamruhusu Ruto arejee Nairobi kufuatia sakata linaloendelea Westgate

23 Septemba 2013

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wanaosikiliza kesi dhidi ya Makamu wa rais wa Kenya William Ruto, wamemruhusu mshtakiwa huyo kurejea nyumbani kwa wiki moja ili kuweza kushughulikia sakata linaloendelelea kwenye eneo la manunuzi la Westgate mjini Nairobi Kenya. Uamuzi huo ulitangazwa haraka mahakamani leo na Jaji Chile Eboe-Osuji ambapo mara moja Ruto alielekezwa kuondoka mahakamani na kupelekwa Uwanja wa Ndege. Waendesha mashtaka hawakupinga uamuzi huo ambapo Ruto amesema kwa hali ilivyo Kenya ni muhimu akawepo.

Jaji Eboe-Osuji ameeleza masikitiko yake na mahakama nzima juu ya kilichotokea Kenya na ametuma risala za rambirambi kwa wafiwa na wananchi wote wa Kenya katika kipindi hiki kigumu. Hata hivyo haijabainishwa iwapo kesi hiyo itaendelea bila ya uwepo wa Ruto.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter