Ban ataka vitendo ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia

23 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amezungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kuchagiza kuimarisha ushirikiano katika kufanikisha kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia na kusema ni muhimu kutekeleza kwa vitendo na sio nadharia pekee ili kutimiza malengo hayo. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema pamoja na kujivunia mafanikio ni muhimu kuongeza juhudi ili kuhakikisha yale yaliyosalia yanatimizwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyobaki.

(Sauti Ban)

"Utaona mafanikio yanayotokana na ushirikiano kutoka wabia wa makundi mabalimbali walikokuja pamoja kwa kuvuka vikwazo dhaniwa. Hata tunaposherehekea mafanikio haya lazima tujifunze katika yale tuliyotimiza na kushindwa ili kuongeza kasi na juhudi katika miaka miwili muhimu iliyosalia."

Ban amewaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba ni muhimu wakaelekeza mitizamo yao katika mikakati na kuhamasisha kutimiza malengo kusudiwa.