Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano baina ya UM na Muungano wa Afrika muhimu: Ban /Nkosazana Dlamini Zuma

Ushirikiano baina ya UM na Muungano wa Afrika muhimu: Ban /Nkosazana Dlamini Zuma

Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika na Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon wakutana kando ya kikao cha baraza Kuu la Umoja wa mataifa.

Viongozi hao wawili wamebadilishana mawazo kuhusu juhudi za kuboresha ushirikiano na operesheni za pamoja za Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika.

Ban amemshukuru Dr. Dlamini-Zuma fkwa jinsi Muungano wa Afrika unazoendelea kuunga mkono kazi za Umoja wa mataifa hususani katika ofisi zake zilizopo Addis Ababa Ethiopia.

Wawili hao pia wamejadili malengo ya pamoja ikiwemo hatua zilizopigwa kama Jamhuri ya Afrika ya Kati , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali, Somalia, Guinea-Bissau, Sudan , South Sudan, pamoja na hali ya Sahara Magharibi.