Ban amelaani vikali shambulio la kanisani nchini Pakistan:

23 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa amelaani vikali shambulio la kigaidi la Jumapili ndani ya kanisa la Kikristo huko Peshawar, Pakistan, ambalo limearifiwa kukatili maisha ya watu zaidi ya 75 na kujeruhi wengine zaidi ya 100 ambao ni wamuni waliokuwa wakihudhuria misa.

Ban Ki-moon amesema shambulio hilo la bomu la kujitoa muhanga ni kitendo cha kikatili kisichokubalika , na anatiwa hofu na kurudia kwa vitendo hivyo ghasia dhidi ya dini na makundi ya wachache nchini Pakistan.

Amesema vitendo hivi vya kigaidi haviwezi kuhalalishwa kwa sababu yoyote ile na ameitaka serikali ya Pakistan kufanya kila linalowezekana kuwasaka na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria wahusika wa shambulio hilo.

Ametoa salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliopoteza maisha na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa kushikamana na serikali ya Pakistan katika vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali na ameitaka serikali hiyo kuendelea kuchukua hatua za kujenga kuvumiliana na kuimarisha ushirikiano baiana ya dini na jumuiya za kikabila nchini humo.