Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la Syria na Libya la tawala mkutano wa Ban na Dr. Nabil Elaraby

Suala la Syria na Libya la tawala mkutano wa Ban na Dr. Nabil Elaraby

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Dr. Nabil Elaraby. Mazungumzo yao yametawaliwa na hali inayoendelea nchini Syria, Libya na hali nzima ya mchakato wa amani Mashariki ya Kati.

Kwa pamoja wamesisitiza haja ya kukomesha umwagaji damu nchini Syria haraka iwezekanavyo pia kushughulikia haraka mahitaji muhimu ya kibinadamu nchini humo.

Katibu Mkuu amekaribisha hatua zilizopigwa na amehimiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa.