Ban azungumza na waziri Wang Yi, wa China

23 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameishukuru serikali ya Uchina kwa jukumu kubwa na mchango wake wa uongozi kwenye masuala ya Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waziri wa mambo ya nje wan chi hiyo Wang Yi, ameishukuru serikali hiyo hususani kwa msaada wa mpango wa ulinzi wa Umoja wa mataifa na mchango wake jatika kuunda ajenda ya maendeleo ya baada ya 2015, kushungulikia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na kufikia maendeleo endelevu.

Ban na waziri huyo pia wamejadili suala la Syria, kuachana na nyuklia kwa rasi ya Korea , na hali ya Afghanistan. Suala lingine ni kubadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa Kaskazi Mashariki mwa Asia.